Kinga ya Muislamu icon

Kinga ya Muislamu

1.0

Bảo vệ Hồi giáo. Dua và Adhkaar.

App Information

Phiên bản
Cập nhật
27 th 04, 2014
Nhà phát triển
Lượt cài đặt
100.000+

App Names

App Description
 
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمن الرَّحيم

Kwa Jina La Mwenyezi Mungu Mwingi Wa Rehema (Duniani) Mwenye Kurehemu (Akhera)
 
UTANGULIZI
Hakika sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, tunamsifu, tunamuomba msaada na tunamuomba maghfirah, tunamuomba Atuhifadhi na shari za nafsi zetu, na maovu ya matendo yetu. Anayemuongoza Mwenyezi Mungu hapana wa kumpoteza, na Anayempoteza, hapana wa wa kumuongoza.  Nakiri kwamba, hapana apasaye kuabudiwa ila Mwenyezi Mungu, hali ya kuwa peke Yake, hana mshirika, na ninakiri kwamba Muhammad ni mja Wake na ni Mtume Wake. Mwenyezi Mungu Amrehemu na Awarehemu jamaa zake na Maswahaba zake na wanaowafuata hao kwa wema mpaka siku ya malipo na Amsalimishe kwa amani nyingi.
Baada ya yaliyotangulia huu ni ufupi (Mukhtasar) wa kitabu kiitwacho “HISWN AL-MUSLIM MIN ADHKAAR AL-KITAAB WA SUNNAH”
Ninamuomba Mwenyezi Mungu kwa majina Yake mazuri, na sifa Zake zilizo juu, Ajaaliye kazi hii kuwa, imesafika  lengo lake, kwa kutaka radhi zake Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Aninufaishe kwa hayo katika uhai wangu huu, na baada ya kufa, na Amnufaishe atakayekisoma, kukichapisha, au aliyekuwa ni sababu ya kukitawanya, hakika  Yeye  Mwenyezi Mungu Ndiye  Muweza.
Mwenyezi Mungu Amrehemu Mtume wetu Muhammad صلى الله عليه وسلم na Aali zake na Maswahaba wake na wanaowafuata hao, kwa wema mpaka siku ya malipo.
Đọc thêm